Kuna
baadhi ya watu wanaogopa kuwa huenda wasiweze kupamba nyumba zao kwa namna
wanayotaka endapo wataamua kujenga kwa kutumia tofali za gharama nafuu. Nyumba
za kisasa za gharama nafuu ni zile zinazojengwa
kwa tofali za gharama nafuu za kupishanisha za hydraform.
Emmanuel
Adauth ambaye ni
mtaalam wa tofali hizi anasema kwamba nyumba hizi zina gharama
nafuu pungufu ya hadi asilimia 30 ukilinganisha na zile za tofali za kawaida za
saruji. Hii ni kwa sababu tofali hizi hazitengenezwi kwa saruji na wala wakati
wa ujenzi hakuna saruji inaotumika kuunganisha tofali moja na jingine.
Nyumba za gharama nafuu zinawezekana
kupendezeshwa kwenye kila eneo hata yale ya usanifu. Kwa mfano uwekaji wa achi
(uwazi, milango au madirisha yenye muundo wa nusu duara eneo la juu)
inawezekana kwa kuzitengeneza sehemu hizo kwa saruji.
Zaidi ya kuwa na kuta zenye tofali
za muonekano wa kuvutia bado mwenye nyumba unaweza kuzipamba kama zilivyo kwa
kupaka polishi maalum tu ama vinginevyo ni kuongezea plasta ya saruji na kupaka
rangi za kawaida. Wapo wanaopendelea kupaka rangi kuta za ndani lakini za nje
wakaacha uzuri wa asili wa tofali kama ulivyo.
Mapambo ya kupigilia ukutani kama
vile saa, fremu na picha yote yanawezekana kwenye kuta za nyumba za kisasa za
tofali za gharama nafuu.
Endapo ulikuwa unasita kwamba
hutaweza kupamba nyumba ya gharama nafuu, kuanzia leo fahamu kwamba si kweli.
Unaweza kupamba ndani na nje kwa kadri unavyotaka.
Vivi anakuwezesha kupamba nyumba yako kwa gharama nafuu kabisa. Tuwasiliane 0755 200023
No comments:
Post a Comment