Hakuna
ubishi kwamba siku maalum kwenye maisha yako zinaweka kumbukumbu za wakati huo.
Na kinachoanza kusema wakati ni saa.
Saa za ukutani
zinaweza kuonekana si chochote kama kifaa cha mapambo ya ndani lakini kama
ukichagua kwa umakini zinaongeza maana ya kuwa matumizi na hapo hapo pambo. Kuna watu ambao wanalijua
hili na wanaweza kuchukua muda mwingi kuhangaika kupata saa zenye muonekano
sahihi wa kuendana na mapambo yao ya
ndani. Saa zikatumika kuwaambia muda na
wakati huohuo zikiongeza mvuto ukutani.
Zifuatazo ni dondoo
za jinsi taa za ukutani zinavyoweza kutumika kama pambo la ukutani:
Unaweza kuweka saa
tofauti na pia zaidi ya moja kwenye kila
chumba.
Saa za ukutani
zenye muonekano wa pambo ziko za mitindo mingi na zinapatikana kirahisi na hata
bei zake sio kubwa, Zipo ambazo fremu zake ni za mbao na zimenakshiwa kwa
mikono, zipo za chuma na zipo za plastiki ngumu. Na hata za madini ya thamani
kama silva huwa zipo. Cha muhimu zaidi
kukumbuka wakati unachagua saa za ukutani zenye muonekano wa pambo, chagua
ambayounajisikia kwamba inakuwakilisha wewe na kwa kiasi fulani inaboresha muonekano
wa chumba chako.
Kutundika saa za
ukutani hakuna tofauti na kutundika fremu za picha au michoro chumbani au
kwenye ujia. Ni sehemu ya mapambo kwa ujumla wake. Kwa ajili saa za ukutani sio gharama kubwa
unaweza kuwa nazo kadhaa. Moja ya mtindo wa kupamba kwa saa za ukutani ni
kuzitundika kadhaa mahali pamoja kwenye mstari. Unaweza kuziwekea muda wa saa
halisi katika miji maarufu ya maeneo tofauti ya dunia. “Watoto wangu wanaishi
ng’ambo na nimeweka saa tatu kuonyesha muda wa Chicago, London na Dar es Salaam
katika mstari mmoja,” anasema Merina Ruge, ambaye ni mkazi wa Kunduchi, Dar es
Salaam.
Kutundika saa
nyeusi kwenye ukuta wenye rangi nyepesi kunatengeneza mwelekeo wa jicho la
mtazamaji.
Muundo wa saa ya
ukutani unachangia muonekano wa pambo, kwa mfano saa ikiwa ya muundo wa
kinyumba cha ndege bila shaka ni ya kipekee. Muundo mwingine wa saa unaoweza
kufikiria ni zile zenye mlango wa mbele wa kioo. Miundo ni mingi mizuri na ya
kipekee kwa mfano zipo saa zinazoonekana kama ni fremu za picha.
Unaweza kutundika
saa kutokana na matumizi ya chumba. Kwa mfano saa ya jikoni unaweza kutundika
yenye muundo wa matunda. Kwa ukuta wa chumba
cha watoto vilevile weka saa zinazoendana na umri na jinsia yao.
Kama umetundika saa
ya ukutani kumbuka unastahili kujua muda kimtindo, na hakuna kizuri zaidi ya
saa sahihi kwako. Kwa muda wa furaha na wa huzuni, saa ya ukutani haikuachi!
Vivi ni mashauri wa
mapambo ya nyumba. Kama kuna lolote linakutatiza kuhusu mapambo ya nyumba na bustani yako wasiliana na mimi. Nimekuwa kwenye huu wigo kwa muda mrefu sasa kwahivyo nina uzoefu wa vingi. Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment