Kwenye majiko yetu wakati wa kuandaa
vyakula kwa ajili ya kupika wengi tunatumia ubao wa kukatia. Zipo mbao za
kukatia zilizotengenezwa kwa malighafi tofauti tofauti kama vile mbao, plastiki
na glasi. Kiafya ubao wa mbao umeonekana ndio unafaa zaidi kuliko hizi nyingine
zote kwa sababu hauwezi kupeleka chembechembe yoyote ya plastiki kwenye chakuwa
kama ambavyo inaweza kutokea kwa ubao wa plastiki.
Hapa tunaangalia namna ya kusafisha
na kutunza ubao huo wa
mbao wa kukatia wakati unapoandaa chakula jikoni.
mbao wa kukatia wakati unapoandaa chakula jikoni.
Osha kwa kusuuza
Tofauti na ule wa plastiki, ubao wa
mbao unatakiwa kuoshwa kwa mithili ya kuusuuza tu kwani mbao ni malighafi asili
ambayo haihimili kusuguliwa kwa nguvu na maosheo makali.
Maosheo magumu kama misugulio itumie
kwenye sinki, sufuria za kushikana na chakula na kwenye vyombo vya plastiki ila
kwa ubao wako wa mbao uoshe kwa kutumia sponji laini, sabuni na maji ya
uvuguvugu.
Usiloweke ubao wa mbao kwenye maji
kwani unaweza kuusababishia kulainika na kuanza kumomonyokamomonyoka.
Matunzo
Kutokana na kwamba mbao ina
vimashimo vidogo ambavyo vinapitisha maji na vitu vingine, ni rahisi vijidudu
kuweka makao. Ili kuua vijidudu vyovyote kirahisi, changanya kijiko kimoja cha vinega
kwenye nusu kikombe cha maji pamoja na limao na sambaza kwenye ubao wako mara
baada ya kuusafisha. Ruhusu ukae kwa nusu saa na ndipo unaweza kuuchukua na
kuusuuza. Uache ukauke kabisa kabla ya kuutumia tena.
Fanya zoezi hili kila baada ya muda fulani
kutokana na matumizi yako hasa kama ubao unakatia kwa wingi vyakula aina ya nyama.
Kama kuna matunda na mbogamboga zimesababisha
ubao wako ukatengeneza madoa tumia chumvi na limao kuusafisha. Nyunyuza chumvi
juu ya ubao halafu isugue kwa limao ambalo limekatwa nusu. Sugulia upande
uliokatwa halafu ukimaliza usuuze na kuuanika.
Kuhakikisha kuwa ubao wako wa
kukatia haubaki na harufu za vyakula tumia magadi soda kidogo na yaache juu ya
ubao usiku mzima. Kesho yake usuuze na kila kitu kitakuwa sawa.
Upake mafuta
Mbao ina vijishimo, ukiwa unaupaka
ubao wako mafuta kabla ya kuutumia kutasaidia kuziba vijishimo hivyo visinyonye
juice/majimaji wakati unapoutumia kukatia vyakula.
Tumia visu vikali
Visu vinahusika moja kwa moja kwenye
ubao wa kukatia. Kisu kikiwa butu kitakufanya ugandamize kwa nguvu wakati wa
kukata, ambapo inaweza kupelekea kuharibu ubao kwa kuutengenezea nyufa.Unaweza
kuepuka hii kwa kunoa visu vyako mara kwa mara na kutumia kisu sahihi kwa kazi sahihi.
Ubao wa kukatia wa mbao unawezesha
visu vyako vibaki kwenye makali muda mrefu zaidi kuliko mbao za glasi, seramiki
au plastiki
Uzuri wa ubao wa mbao wa kukatia
haupingiki. Ni rafiki kwa visu vyako, ni salama kwa familia yako na pia ni
vyema kuunga mkono vya kwetu kwa kutumia bidhaa hii inayotengenezwa na
wajasiriamali wadogo!
No comments:
Post a Comment