Kila
kona ya chumba iliyo tupu ni fursa yako kubuni namna ya kuipendezesha. Na
wakati unaipendezesha unaweza kujikuta unaitumia pia. Mara nyingi kona zimekuwa
zikisahaulika au kudharaulika, ukitaka uitumie kona ipasavyo ni pale unapokuwa
na nyumba ndogo huku unahitaji kunufaika na kila eneo na pengine una vitu vingi unavyohitaji kuviweka katika
mpangilio ili nyumba yako iwe na
muonekano wa kuvutia.
Endelea kusoma makala hii ufahamu njia za kuifanya kona iliyo tupu
ipendeze na kutumika kwa manufaa zaidi.
·
Weka
shelfu za vitabu ambazo zimetengenezwa kwa muundo wa kufuatisha kona ilivyo.
Hii ni moja ya njia nzuri za kufanya kona isiyokuwa na kitu iweze kutumika na
shelfu zinaweza kwenda hadi juu kabisa karibia na dari hata kama utapanda juu
ya kitu wakati wa kuchukua kitabu kilicho shelfu la juu zaidi.
·
Mbali
na shelfu za vitabu unaweza pia kuweka shelfu kwa ajili ya kuonyesha mapambo
mengine madogodogo na hata mimea midogo ya urembo.
·
Tundika
bembea la kumpembelezea mtoto. Unajua jinsi nyumba yenye mtoto wa kubebwa
inavyokuwa na msongamano wa viti vya kubembea sakafuni. Unaweza kuondokana na
msongamano huo kwa kununua bembea na kulitundika kwenye kona. Licha ya bembea
husika kuwa la mtoto hata wewe mtu mzima unaweza kubembea pale anapohitaji kujiburudisha kidogo.
·
Fanya
kona iwe kituo cha kufanyia kazi zako za kiofisi kwa kupatengenezea dawati na kiti.
Hakuna eneo zuri la kufanyia kazi kwa kutuliza akili kama ambalo macho hayakutani
na usumbufu. Kwa mkao huu wa kwenye kona ni kwamba macho yako yanatazama moja
kwa moja kwenye kazi yako au ukivuta pumzi unayaelekeza ukutani. Vilevile ni njia
ya kufanya kona iwe kituo cha kuwekea vitu vya kukuwezesha kuwa na mpangilio.
Kwa mfano sehemu ya kuwekea nyaraka, kalamu au kuchajia vifaa vya elektoniki, huku eneo la juu ukiweka mbao za kutobolea
karatasi za ujumbe mbalimbali kama vile ratiba za mapishi na usafi wa nyumba.
·
Ifanye
kona iwe eneo la kutundika picha za familia. Huhitaji ukuta mkubwa kwa ajili ya
kusambaza picha za familia yako badala yake tumia kona kuongeza mvuto.
·
Weka
mmea mkubwa unaofaa kuoteshwa ndani hapo kwenye kona kama hutataka kuweka
shelfu au sanaa zozote. Hii itasaidia kuingiza uoto asili ndani ya nyumba huku
matawi yake yakitumika kuijaza kona yenyewe.
·
Tumia
kona kutengeneza eneo la kutundikia nguo, hasa kwenye chumba cha kunyooshea au
cha wageni kwani mara nyingi vyumba hivi ni vidogo kwahivyo pachika fimbo
itakayokutanisha pande mbili za kuta za kona kwa ajili ya kutundikia nguo, kutumia
kona kwa shughuli hii ni matumizi mazuri ya chumba husika.
·
Tumia
kona kutengeneza eneo la kuhifadhia michezo ya watoto
·
Weka
sofa la duara au lenye vipande viwili ambavyo vitaunganikia kwenye kona.
·
Weka
meza ya duara. Meza ya duara inakaa watu wengi kuliko ile ya pembenne.
Inapokuwa karibu na kona eneo linafiti vizuri kuweka kiti cha kukalia, na
kikiwa ni cha mgongo mrefu kona inapendeza zaidi.
·
Pendezesha
kona kwa kuweka vinyago vikubwa.
·
Patengenezee kabati
au kimeza cha kona chenye miguu mitatu. Bila shaka utakapomtafuta fundi mzuri
ana uwezo wa kuchukua vipimo vya kona yako na kukutengezea fenicha ya kufiti
hapo vizuri kabisa. Na pia sia ajabu kwenye maduka ya fenicha kukutana na
kimeza au kabati la aina hii ambalo
litatosha kwenye kona. Kuna sababu ya kwanini hizi fenicha za hivyo
zinatengenezwa.
Kwa dondoo za kupendezesha nyumba nifuate instagram @vivimachange
No comments:
Post a Comment