kupe mkubwa |
WANAWAKE wa Kimasai wanaopinga suala la tohara kwa watoto
wamegundua njia nyingine ya kukabiliana na
ukeketaji kwa kutumia kupe wakubwa.
Hayo yalielezwa katika warsha ya kujipanga kupokea mradi wa
kijiji cha dijitali, iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan hivi karibuni.
Wakijadili changamoto ya ukeketaji kama sehemu ya shida
kubwa ya jamii kiafya, wanawake wamesema kwamba hukamata kupe wakubwa na kuwaua
kisha kupiga vigelegele kuonesha kwamba mabinti wao wamepewa tohara.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo alipouliza inakuwaje hapo
baadaye binti anapokuwa mkubwa, aliambiwa kwamba ni rahisi kwa binti huyo hapo
baadae kuzungumza na mwenzake wakaelewana.
“Tatizo la tohara ni la wanaume, wanaume hawa ndio
wanahimiza wanawake wawe na tohara kwa kuwa wanataka kuwaoa wanawake ambao
wameingia tohara kama wao,” alisema mama mmoja.
Alisema namna hiyo imefanya kuwakwepesha mabinti wengi na
vurugu za tohara, ambazo kiafya si sawa, hasa kutokana na tatizo linaloambatana
na kovu wakati wa uzazi na pia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa upande wa mwanamke.
No comments:
Post a Comment