Sebule, nilichojifunza kwake ni kwamba pamoja na kupenda kumachi ila pia hapendi makorokoro mengi sebuleni. Sofa lake moja la nusu duara linamtosha. Sofa round na coffee table round...shape neighborhood
Dining room yake ndogo kila kitu elegant, meza ya marble, wall art, viti na carpet maridadi kabisa. Pia hapa fahamu kuwa meza ya marble kwa asili yake imeshakuwa decorated tayari. Kwa maana hiyo huhitaji kuifunika na vitambaa tambaa. Hapa kaweka tu center piece yake simple.
Angalia ujirani wa rangi unavyopendeza, pink inagusa kwenye maua ya kwenye vesi, maua ya kwenye shower curtain na carpet bila kusahau taulo. Nimemkubali kwa decor ya match match. Mama mwenye nyumba wa aina hii ni yule anaenda shopping ya decor zake akijua kabisa kichwani ni nini anataka na hayumbishwi na vingine asivyovihitaji.
Sanaa ya ukutani ipo mahali pake na kwa size yake imefiti kabisa kwenye huo ukuta kwani si ndogo sana wala kubwa zaidi.
Bathroom nyingine hii, taulo, trash can na carpet ni mwendo wa kumechisha tu. Nzuri sana kwakweli....
No comments:
Post a Comment