Ni kweli kuwa kuna watu wengi tu hawapendi vipande vya
barafu vya kawaida kwani vinayeyukia kwenye vinywaji vyao na kufanya ladha iwe
dhaifu kuliko ambavyo ingetakiwa iwe.. Habari njema ni kwamba kuna
mbadala
ambao ni vipande vya barafu za kutumia zaidi ya mara moja.
Vipande
vya barafu vinavyotumika zaidi ya mara moja (reusable ice cubes) ni vidude ambavyo vimetengenezwa kwa malighafi
tofautitofauti ila vingi vikiwa ni vya plastiki, ambapo ndani yake kimewekwa
maji safi ya kudumu ambayo ndio yanaganda kwa ajili ya kufanya barafu.
Barafu
za kutumia zaidi ya mara moja zipo za miundo mbalimbali na yakuvutia kwa mfano
pembe nne, samaki, vipande vya matunda na mingine mingi cha muhimu tu ni kwamba
vyote hivyo vinagandishwa na kutengeneza barafu. Pia rangi zake zaweza kuwa
bluu, njano na nyeupe.
Barafu
hizi ni sahihi kwa wale ambao hawana haraka na vinywaji vyao. Hii ni kwasababu
haziyeyuki haraka kwani barafu iko ndani lakini nje ni plastiki. Barafu hizi
pia ni muhimu kama ifuatavyo:
Zinafanya kinywaji kuwa baridi bila kuyeyukia ndani yake.
Hazifanyi kinywaji chako kipoteze ladha. Hii ni kwakuwa hakuna maji yanayoingia
kujichanganya kwenye kinywaji chako kama zile barafu nyingine za kawaida ambazo
zinayeyukia ndani na hivyo kuondoa ladha halisi. Na wengi wanapenda vinywaji
vya baridi ila inaonekana kuwa wanachukia vipande vya barafu vya maji kwani
vinayeyukia ndani ya kinywaji na kukipunguzia ladha yake ya mwanzo.Kama wewe ni
mmoja wao basi tumia reusable ice cubes.
Barafu hizi unaweza kuzitumia tena na tena, unachotakiwa
tu ni kuwa baada ya kutumika zioshe,
zifute na kuzigandisha tena. Zihifadhi kwenye friza kwa ajili ya kutumia wakati
wowote.
Barafu za kutumia zaidi ya mara moja nyingi ni za
plastiki au malighafi nyingine na ni za kutengeneza kiwandani ambapo
zinaonekana kama barafu za maji yaliyoganda (za siku zote zilizozoeleka ziadi)
ila ndani yake kuna maji ambapo unaweka kwenye friza na ndipo hayo maji ya ndani
yanaganda.
Umuhimu wake hapa ni kuwa na matumizi mazuri ya maji, yaani huna
haja ya kujaza maji kugandisha barafu kwani maji ya kudumu yako kwenye hivi
vidude tayari.
Na licha ya haya matumizi mazuri ya maji bado wakati mwingine
huna uhakika juu ya usalama wa maji yaliyotengengenea barafu za kawaida kama
hukuyaweka mwenyewe.
Barafu hizi ni za kudumu. Endapo hivi vidude havitapasuka
maji yake ya ndani yapotee basi unaweza kuvitumia maisha yako yote na hata
vizazi vya mbele yako.
Barafu za kutumia zaidi ya mara moja zinasaidia kukifanya
kinywaji kiwe baridi kwa asilimia 20 zaidi ya barafu za kawaida.
Kama
bado huna nenda kanunue, zinauzwa madukani. Ni nzuri sana kwa nyumbani na
kwenye sherehe.
Na kama ulikuwa
hujui basi ukialikwa kwenye kimnuso ukakutana na hivyo vidude, fahamu ni reusable ice cubes kwa hivyo chota
upooze kinywaji chako.
Nawe msomaji nishirikishe uvumbuzi wowote uujuao kuhusu
maisha yako ya kila siku hapo nyumbani kwako. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri. Piga/Whatsapp 0755 200023
No comments:
Post a Comment