Rangi sahihi zitakifanya chumba cha wakuu wa
familia kama mahali patakatifu. Kuchagua rangi kwa ajili ya kupaka chumba cha
wazazi (master bedroom) ni moja kati ya hatua kubwa unazochukua wewe
mwenyenyumba za kutengeneza mahali binafsi. Chaguo lako linatakiwa
liendane na
muonekano wako kwa jinsi ya mtindo wako wa kupamba. Kwakuwa nyumba
kwenye nyumba nyingi za kisasa chumba cha wakuu wa familia ni kikubwa kuliko
vyumba vingine, una machaguo mengi na unaweza kuchanganya rangi tofauti kwenye
kuta nne za chumba hiki ile kuleta muonekano wa kipekee.
Kama chumba cha wakuu wa familia kimeungana na
bafu na sehemu ya kuvalia inakubidi kuweka mpangilio wa rangi kwenye maeneo
hayo yote. Hii haimaanisha kuwa rangi ya chumbani na bafuni zinapaswa kufanana,
bali inamaanisha zinapaswa kushirikiana. Kuchukua rangi moja kutoka sehemu moja
na kuleta mguso wake kwenye sehemu nyingine kutatengeneza chumba cha kuvutia.
Fikiria mandhari unayotaka kuitengeneza
chumbani. Wenye nyumba wengi wanataka mandhari tulivu ya rangi nyepesi. Japo
hii haimaanisha kwamba rangi za kuwaka au nzito hazina nafasi kwenye chumba
chako. Kama unadhani unazipenda rangi hizi (za kuwaka na nzito) basi fanya
kuchanganya kuta na zile tulivu na nyepesi badala ya kupaka rangi moja chumba
kizima.
Mara baada ya kuamua ni rangi zipi unataka
kupaka, kinachofuata ni kufikiria jinsi gani unataka kuzitumia. Kama unataka
rangi ya kuwaka kwenye chumba chako fikiria kijani. Je, unaipenda kijani?
Kijani kama cha tunda la epo kina nadharia ya kuwaka na tulivu ambapo kijani hiki
unaweza kukichanganya na rangi tulivu kama vile krimu nyeupe.
Vilevile bluu ya
mawingu nayo ni tulivu na laini kwa chumba cha kulala. Kuna jamii nyingi za
bluu nyepesi kwa ajili ya kuta za chumba cha kulala endapo hutaki ile bluu
nzito. Bluu nyepesi zinafanya vizuri zikichanganywa na kahawia endapo nia yako
ni kuchanganya nyepesi na nzito. Laa kama unataka kuchanganya nyepesi kwa
nyepesi basi nyepesi ya bluu inaendana na nyeupe. Usishange kwanini mawingu
yanapendeza! Vilevile bluu na kijani nyepesi zinapendeza zikitumika pamoja.
Kama
nyekundu ndio rangi unayopendelea zaidi, unaweza kuitumia kwenye chumba cha
kulala, ila kwa tahadhari. Nyekundu inaleta mhemko na ikiwa nyingi inaweza
kuchosha mwili.
Ama chagua nyekundu iliyofifia au paka kwenye ukuta mmoja tu,
ule ukuta wa tendego (ubao wa kichwani
wa kitanda) au ule wenye dirisha kubwa , ili mwanga upunguze makali ya rangi.
Kuta tatu zilizobakia paka nyepesi ya kati ya zilizoainishwa juu.
Dondoo
ya nyekundu inatumika vilevile kwa njano na chungwa. Hata nyeusi inawezekana
kwenye chumba chako cha kulala ila kuwa makini kuichanganya na nyeupe na utaratibu
ni uleule wa kuipaka kwenye ukuta mmoja tu kama ilivyoainishwa kwenye nyekundu.
Kupata ushauri wa mapambo ya nyumba na bustani tuwasiliane
0755 200023
No comments:
Post a Comment