Saturday, January 9, 2016

VML:......MENU YA WANAOFANYA DIET NA JINSI YA KUSAFISHA UBAO WA KUKATIA


Hii menu ni kwa hisani ya instagram ya
sherry_kitchenHealthy eating..DINNER KWA DIETERS

CHAKULA: Salad ya mafuta na kuku
Unahitaji:

Tango laini 1
Hoho ya kijani (green bell pepper) 1
Nyanya 3 medium
Green onions 2
Kipande kimoja cha kidari cha kuku (kata kama kwenye picha)
Robo kikombe cha giligilani
Nanaa (mint) ¼ kikombe
 
Mafuta ya zaituni (olive oil ) ¼ kikombe (punguza ukipenda)
Limao kijiko 1 cha chakula
Lettuce (majani ya salad) kiasi
Chumvi kdg
Kijiko 1 cha chakula cha sumac/shimak ilosagwa
 
Njia:

Katakata vitu vyote vikubwakubwa isipokuwa kuku fanya kama nlivoeleza juu. Weka mafuta kwenye sufuria na yakipata moto weka kuku na umkaange mpk akauke na kuiva vzr. Weka vitu vyote isipokuwa limao na sumac spice na ukoroge kwa dk 1.

Opoa. Kisha changanya sumac spice na limao mpk ichanganyike vzr. Tia kwenye salad na uifurahie.

Alternatively unaweza kum grill kuku wako na kumkata vipande vdgvdg. Endapo utafanya hivi basi tumia vijiko 2 tu vya mafuta.
Tamu sana sana sana
😍
Kata kipande cha limao halafu kichovye kwenye chumvi na sugua taratibu ubao wako wa kukatia, ni ubao uliotengenezwa kwa malighafi zozote uwe ni mbao au plastiki. Baada ya hapo malizia kwa kuosha kawaida kwa osheo sabuni , maji na kuufuta. Kusafisha kwa njia hii japo mara moja kwa wiki kuendana na matumizi ya ubao kunasaidia kuua vijidudu na bakteria.

Nawe msomaji kama kuna dondoo ya maisha ya nyumbani unayoifahamu usisite kunitumia. Yoyote kuhusu chochote na inaweza kuwa hata mstari mmoja au miwili. Piga/whatsapp 0755 200023


No comments:

Post a Comment