Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua
unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho
ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.
Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha
anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi.
Kina pia teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na
virusi.
Licha ya choo hicho kuuzwa $9,800 (£6,704),
waliotengeneza choo hicho vyoo zaidi ya 40 milioni vya miundo ya awali
vimeuzwa.
Kampuni ya Toto, iliyotengeneza choo hicho, imesema
muundo huo wa sasa bado unaendelea kuboreshwa.
"Huhitaji kuosha bakuli la choo kwa kipindi cha
mwaka mmoja,” anasema msemaji wa Toto, Bi Lenora Campos.
Choo hicho hata hivyo si kwamba kitakuondolea kabisa
majukumu yote ya usafi chooni, kwani hakiwezi kujiosha upande wa nje iwapo
kutakuwa na uchafu.
Maonyesho hayo ambayo kwa Kiingereza yanajulikana kama
Consumer Electronics Show hufanyika kila mwaka ambapo kampuni mbalimbali na
wavumbuzi huonyesha teknolojia za karibuni zaidi.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment