Friends, hebu tutazame picha za vyumba hizi tujifunze kitu. Tusijali kama ni mazingira ya uzunguni kwani hata sisi kibongobongo inawezekana...binadamu ni mmoja mazingira ndio tofauti.
Hapa nataka tuangalie hiki kizulia cha jikoni. Miguu inaburudika kukanyaga zulia hasa pale inaposimama muda mrefu. Kwa jikoni unaweza kutupia kizulia maeneo kama kwenye sink na cooker. Kama jikoni kwako tayari umeshatupia tafadhali nitumie picha..
Hapa katika hii meza ya chakula nataka uone namna nyingine ya kutumia table runner. Wengi tumezoea ile runner ya kupita kati tu, kumbe unaweza kutupia runner mbili, tatu au nne kuendana na ukubwa wa meza yako zikawa na kazi 2; mapambo na mats.
Hiki chumba cha watoto wa kiume ona jinsi vitanda simple kabisa vya chuma vilivyokaa vizuri. Wakati mwingine nyumba kupendeza si pesa ndefu bali ni ubunifu na kuwa na fikra pana hasa kujitahidi kujua option nyingi kabla hujaamua jambo. Na hapa ndipo unakuja umuhimu wa ushauri wa mtaalam. Kitanda kimoja kama hiki kinaweza hata kisifike laki na nusu.
Pata ushauri wa busara kabisa wa mapambo ya nyumba na bustani yako toka kwangu..Let's meet 0755 200023
No comments:
Post a Comment