Neema akiwa na mbwa wake scooby kwenye gari. Anasema scooby ni mpole anasafiri naye hahangaiki, mkewe ni mjamzito kwahivyo anategemea kupata wajukuu soon..lol
Binafsi kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara ni kwamba sipendi mbwa, lakini navutiwa kusikiliza stori za wanaomiliki mbwa ili kujua kwanini wanafanya hivyo. Hapa kuna hii stori toka gazeti la mwananchi inayosema..VENANCE MWAMOTO: Baada ya kukosa ubunge nilifuga na kuuza
mbwa
Tumezoea kuona mbwa akifugwa katika nyumba nyingi kwa
lengo la kusaidia ulinzi katika nyumba hiyo. Agharabu wengine hupendelea kufuga
mnyama huyo kama rafiki pia kama pambo. Hali ni tofauti
kwa mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto ambaye ameamua kufuga mnyama huyo
kwa ajili ya biashara na huwatunza kisha kuwauza kwa lengo la kujiongezea
kipato.
Mwamoto
ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 anasema,
alianza ufugaji baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.“Katika maisha yangu siku zote
nimezoea kufanya shughuli mbalimbali kwa lengo la kujiongezea kipato na siyo
kubweteka na kusubiri kazi moja, ndiyo maana najishughulisha na kilimo na
ufugaji.Mwamoto anasema,
alianza kufuga mbwa wawili wa jinsi tofauti na baada ya muda waliongezeka na
kuwauza.
Anasema anawauza
mbwa hao, Rwanda na Burundi pamoja na kwenye kampuni za migodi. Mbwa mkubwa
huuza kwa Dola za Marekani 800 sawa na Sh1,400,000 za wakati kwa wadogo huwauza
kwa Dola 200 (Sh450,00).Mwamoto anasema mbwa anaowafuga ni maalumu kwa ajili ya ulinzi na
inamlazimu kuwapa mafunzo maalumu tangu wakiwa wadogo.
Hata hivyo, hakuna kazi isiyokuwa
na vikwazo, Mwamoto anasema changamoto kubwa anayokumbana nayo ni kebehi,
kusema vibaya na kuchekwa, huku wengine wakimhusisha na kula nyama ya mbwa.“Mimi ni Mhehe watu wengi
wanaamini sisi tunakula mbwa, hivyo napata wakati mgumu kwani watu wananikebehi
na kunikashifu kuwa nafunga mbwa kwa ajili ya chakula, lakini hilo halinivunji
moyo na naichukua hiyo kama changamoto ya kuongea juhudi zaidi.”
Kama na wewe unamiliki mbwa hebu nishirikishe je ni wa pambo, hobby mlinzi au biashara? Tuwasiliane 0755 200023
No comments:
Post a Comment