Friday, March 27, 2015

CISSY HOUSTON: Tuko tayari kwa kifo cha BOBBI KRISTINA BROWN...........wenyewe wanapenda kumuita Kriss

KADRI hali ya mtoto wa aliyekuwa nguli wa muziki nchini Marekani, Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown, inavyozidi kuwa mbaya, ndugu zake wametangaza kuwa tayari kupokea taarifa za kifo chake.
Jana bibi wa binti huyo, Cissy Houston, aliweka wazi kwamba familia ya binti huyo na ndugu kwa ujumla imeshajiandaa na mazishi ya binti huyo, hivyo ipo tayari kupokea taarifa yoyote kuhusu binti wao.

“Familia imejiandaa kwa mazishi ya mjukuu wangu kwa kuwa hadi leo hawajui hatima yake kutokana na hali yake kuwa mbaya tangu Januari 31 mwaka huu, licha ya kuwa katika uangalizi wa madaktari nguli,’’ alisema bibi huyo.

“Kwa hali iliyopo kwa sasa kila kitu tunamuachia Mungu, labda maajabu yatokee, lakini tupo tayari kwa lolote kwa sasa, tunawashukuru watu wote ambao wanaendelea kumuombea mtoto wetu, japokuwa bado hali yake haieleweki.

“Kama atapona, tutamshukuru Mungu, familia tunaendelea kumuombea lakini bado hali yake haijabadilika na inazidi kuwa mbaya.”

No comments:

Post a Comment