Monday, March 30, 2015

RANGI ZA MAZULIA YA NYUMBANI NI NYINGI........UNAAMUAJE UNUNUE RANGI IPI..?

Hakuna sakafu inayoipa miguu ulaini kama sakafu ya carpet. Carpet linafanya sakafu salama kwa watoto kucheza na pia linapunguza uwezekano wa kuumia wanapoanguka. Ni kweli carpet linahitaji utunzaji wa ziada ukilinganisha na sakafu nyingine kwa mfano za tiles, mbao, tarazo nk.

Kwa rangi lukuki zilizopo, inaweza kukuwia vigumu kuchagua rangi sahihi kwa ajili ya nyumbani kwako. Rangi nyingine kama cream na nyeupe, light blue yani kwa ujumla rangi za mwanga zinahitaji usafishaji na utunzaji wa ziada. Rangi za giza kama brown, nyekundu na maroon hazihitaji usafishaji wa mara kwa mara kama zile za mwanga, ila kuwa makini kwani rangi za giza huwa zinapauka.

Sasa uamuzi ni wako, unadhani ni rangi zipi za carpet zinakufaa zaidi...za mwanga au za giza?

No comments:

Post a Comment