Tuesday, March 31, 2015

SAKATA LA KUTAKA KUUAWA DK SLAA.......................MCHUMBA WAKE ATOA MAELEZO

MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, Josephine Mushumbusi jana ametoa maelezo yake katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kuhusu tuhuma za kutaka kuuawa kwa katibu huyo.

Akiwa amefuatana na Dk Slaa, Mushumbusi alifika kitu kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kutoa maelezo kwa saa mbili.

“Nimekuja kutoa maelezo yangu, sikuwa na mengi ya kusema zaidi ya kile ninachokifahamu,” alisema na kusema wakati mwito ulipotolewa kwenda kutoa ushahidi, hakuwa nchini.

Dk Slaa alisema, Mushumbusi amemaliza kazi yake ya kutoa maelezo na taarifa waliyoipata ni kuwa mashahidi wamemaliza kutoa ushahidi wao, hivyo wanasubiri hatua zaidi.

“Mama alikuwa anatoa ushahidi na amemaliza kazi yake, lakini ikumbukwe huyu siyo mtuhumiwa hajaja kuhojiwa ila ni shahidi, kwa sababu ukisema kuhojiwa ina maana ni mtuhumiwa,” alisema Dk Slaa.

Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa madai kwamba aliyekuwa mlinzi wa Dk Slaa, Khalid Kagenzi, alitaka kumwekea sumu Katibu Mkuu huyo.

Hata hivyo, Kova alipoulizwa kuhusu kuwepo Mushumbusi kituoni hapo kutoa maelezo yake, alisema hana taarifa yoyote na hata kama akiwepo, ni hali ya kawaida.

Alisema ingekuwa ni jambo tofauti au kubwa angepata taarifa lakini kitendo cha mtu yeyote kuitwa kutoa maelezo ni cha kawaida.
CHANZO: HABARILEO

No comments:

Post a Comment