Monday, March 23, 2015

SIDIRIA YATUMIKA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA

Mwanamke mmoja muuzaji dawa za kulevya anakabiliwa na adhabu ya kifungo baada ya kukutwa akiwa amesheheni dawa za kulevya aina ya Cocaine katika sidiria yake yenye kipimo cha ukubwa wa 46d.
Nola Williams,mwenye umri wa miaka 47,alisimamishwa katika uwanja wa ndege wa Gatwick ,akitokea Jamaica akiwa na mtoto mdogo pamoja na muuza unga mwenziwe aitwaye Raymond Goodison mwishoni mwa mwezi january mwaka huu.

Williams and Goodison alikamtwa na polisi alipokuwa akitaka kupanda ndege kutoka uwanja wa ndege wa Gatwick kuelekea Victoria mji ulioko kati kati mwa London.

Tukio hili limeng’amuliwa na polisi walipokuwa wakifanya ukaguzi kwa wasafiri na hivyo kugundua kilo moja ya cocain ikiwa imeshonewa kwenye sidiria ya Nola .

Goodison, alikuwa akikabiliwa na makosa kama hayo ya usafirishaji mihadarati aliachiliwa baada ya kulipa fidia na kuikimbia Uingereza hapo awali.


washirika hao wa sidiria

Nola Williams anasubiri kifungo chake ,wakati Goodison alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na mitatu jela .

Na inasemekana kwamba Raymond alimtumia bi Nola kuingiza dawa za kulevya katika sidiria yake,bila wasi wasi Nola alikwenda katika viwanja hivyo vya ndege akiwa na mtoto mdogo na ndipo alipogundulika kuwa ameficha dawa hizo katika sidiria yake.


Williams,ni mkaazi wa Stockwell, London kusini,amekubali makosa yake ya kusafirisha dawa za kulevya ,lakini kifungo chake kilicheleweshwa, wakati mwanasheria wake akilalamika kuwa mteja wake ambambikiwa kesi hiyo na kusema kuwa mwanamke huyo kosa linalomhusu ni usafirishaji binaadamu na sio dawa za kulevya. Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment