Tuesday, March 24, 2015

ANGELINA JOLIE AONDOLEWA NYUMBA YA UZAZI KUTOKANA NA TISHIO LA SARATANI........Kuweza kusema hili hadharani kutawaokoa wanawake wengi

Muigizaji Angelina Jolie amelazimika kutoa mishipa ya kupitisha mayai na vifuko vya mayai baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.

Muigizaji huyo maarufu wa Hollywood ameidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa uzazi wake juma lililopita katika upasuaji wa dharura.

''Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani'' alisema Bi Jolie

Habari hizi zimewashtua wafuasi na mashabiki wa totoshoo huyo ambaye miaka miwli tu iliyopita alilazimika kukatwa matiti kwa sababu ya tishio hilohilo la Saratani.

Aidha mamake muigizaji huyo nyota aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.

''Sio jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu'' alisema Jolie.

Jolie ambaye ni mkewe muigizaji nyota wa Holywood ctor Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.
Wawili hao wanawatoto sita.

Mamake tayari aliaga dunia kutokana na Saratani

''Nilimpigia simu akiwa Ufaransa na akarejea nyumbani mara moja ,lakini cha msingi ni kuwa ukikabiliwa na masaibu kama haya ya kiafya na uwe una mtu anayeweza kukusaidia kwa kukuchangia mawazo mzigo unakuwa mwepesi zaidi''

''Mamangu aligunduliwa kuwa na saratani akiwa na umri wa miaka 49 hivi sasa nina miaka 39 ''

''Licha ya hayo hivi sasa nimeshakoma kuzaa kwa hivyo ninatarajia mabadiliko mengi katika mwili wangu .Hivi sasa sina hamu ya kupata watoto wengine ,alisema jolie.

“Nitastahimili kwa njia ileile ambayo nafikiri maelfu ya wanawake wamepitia''


''Nilijiambia mwenyewe ni lazima nijikaze na kuwa na nguvu maanake sikuwa na sababu ya kujifikiria mimi bila kuona watoto wangu wakijuta na kusema looo! mamangu alikufa kutokana na saratani ya nyumba ya uzazi'' alisema bi Jolie.

No comments:

Post a Comment