Friday, March 27, 2015

ASKOFU GWAJIMA AMEJISALIMISHA POLISI LEO KUHOJIWA KUTOKANA NA KUTOA LUGHA CHAFU DHIDI YA KARDINALI PENGO

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima leo amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.


Gwajima alirekodiwa kwenye ibada ya kanisa lake
Jumapili iliyopita ambapo ‘alimtusi’ Pengo akituhumu kuwa ni msaliti kwani amekwenda kinyume na Taasisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kuwataka waumini waisome Katiba Inayopendekezwa kisha wapewe uhuru wa kupiga kura ya “ndiyo” au “hapana” tofauti na vyombo hivyo vyenye dhamana ya kuongoza dini ya Kikristo vilivyotaka waumini waipigie kura ya “hapana” Katiba Inayopendekezwa.
CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment