Sunday, March 29, 2015

SWALI KWA WANANDOA..

Nimekutana na hili swali kwa wanandoa Jamiiforum nikaona si mbaya niliweke hapa.

Mke alimuomba mume ampe lifti mpaka kwenye sherehe ( kitchen party, mume akasema yuko busy ofisini ila akampa hela ya taxi. 

Alipofika kwenye sherehe akakutana na msichana mrembo wakazoeana na kuanza kubadilishana story za hapa na pale.


Sherehe ilipoisha waliulizana njia ya usafiri ambayo kila mmoja atatumia kuondoka. 
Yule mke wa jamaa akasema yeye amepewa hela ya taxi kwa hiyo angetumia taxi kurudi nyumbani.

Yule binti mrembo akasema aliletwa na "boyfriend " wake hivyo angekuja kumchukua. Hivyo akamwomba rafiki yake huyo asitumie taxi .

Baada ya muda mfupi gari ya boyfriend wa yule binti mrembo likaingia. Yule mama akakaribishwa apande , alipotahamaki akagundua ni gari ya mume wake. 


Akapanda kiti cha nyuma na akatambulishwa kama rafiki wa yule binti mrembo. Mume alipogeuka akakutana uso kwa uso na mkewe!

Swali: ungekuwa wewe (mwanamke au mwanaume) ungefanyaje?

No comments:

Post a Comment