Friday, March 27, 2015

Watanzania mnashauriwa KUACHANA NA MITUMBA..............WOOLWORTHS DAR ES SALAAM WAMETOA PUNGUZO LA ASILIMIA 50 MSIMU WA PASAKA......PUNGUZO LITADUMU KWA WIKI 4

   
WATANZANIA wameshauriwa kuachana na matumizi ya nguo zilizotumika maarufu kama mitumba ambazo tayari baadhi zimeonekana kuwa na madhara  mbalimbali ya kiafya yanayotokana na matumizi ya nguo hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa punguzo la asilimia hamsini kwa nguo katika duka la Woolworths kwa ajili
ya sikukuu ya Pasaka jijini Dar es Salaam jana, mkurugenzi wa duka hilo Joehans Bushiri alisema nguo za mtumba si salama kwa matumizi kwa kuwa tayari zimeshatumika.

Alisema kuwa kwa kutambua hali hiyo tayari Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa likitoa tahadhari kuhusiana na matumizi ya nguo hizo ikiwa ni pamoja na kufanya operesheni mbalimbali za kuwakamata wafanyabiashara.

“Tunawasihi Watanzania kuepukana na matumizi ya nguo za mtumba kwani si salama kwa afya zao. Katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka duka la Woolworths linatoa punguzo la asilimia hamsini ili kuwawezesha Watanzania kupata nguo mpya na zenye ubora.Punguzo hili titadumu kwa wiki nne,” alisema.

Bushiri alisema duka hilo ambalo ni moja kati ya maduka makubwa ya nguo hapa nchini,litaendelea kuwahudumia wateja wake kwa kuwaletea nguo nzuri kwa kutoa punguzo katika msimu huu wa Pasaka na kwa gharama nafuu.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa,duka hilo pia linatoa nafasi kwa wateja kununua nguo kwa kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi mitatu ili kuwawezesha wale wasio na fedha za kutosha kwa kulipa mara moja kupata nguo nzuri pamoja na mahitaji mengine.

Kuhakikisha wateja wetu wanapata vitu bora kabisa, vinavyoendana na wakati na kwa muda mwafaka, Woolworths imeweza kubadilisha mfumo wa uletaji wa bidhaa nchini badala ya kutumia meli kama zamani sasa inatumia usafiri wa ndege. Kabla ya hapo tulikuwa tunatumia muda wa mwezi mmoja hadi miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa tunatumia muda wa wiki mbili hadi tatu.

Bw. Bushiri pia akasisitiza kwamba anapenda kuwahakikishia wateja wao kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote kama zinazopatikana Afrika ya Kusini na kwa bei zinazofaa kabisa.


Alisema kuwa punguzo la bei limekuja kipindi kizuri ambacho familia zinafanya manunuzi kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.
CHANZO: MAJIRA

No comments:

Post a Comment