Monday, March 30, 2015

HATIMAYE OBAMA KUZURU ALIKOZALIWA BABAKE JULAI MWAKA HUU

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Barrack Obama atazuru Kenya mwezi Julai mwaka huu, taifa alikozaliwa babake.

Inasemekana kuwa Bwana Obama, atahudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu ujasirimali, utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo-Nairobi.

Tangu awe Rais wa Marekani, Barack Obama hajawahi kuzuru taifa hilo la Afrika Mashariki kama Rais.

Alizuru mataifa kadhaa za Afrika ikiwemo ziara ya taifa jirani Tanzania mnamo mwaka 2013 bila kuzuru Kenya.

Alizuru Kenya akiwa seneta mnamo mwaka 2006.


Bababke Obama alisomea Marekani na hatimaye kurejea Kenya baada ya Obama kuzaliwa.
CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment