Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
|
-Akutana na viongozi wa dini kwenye hifadhi za Tarangire, Arusha
-Wamtaja kwa sifa zinazolenga `kumpigia debe` la kuchaguliwa

Haijawahi kutokea!
Ndivyo inavyoweza kutafsiriwa wakati
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipofanikisha ziara ya
viongozi takriban 58 wa madhebu tofauti kutembelea hifadhi ya Tarangire mkoani
Manyara na kufanya nao mazungumzo kwa nyakati tofauti.Ni ziara iliyoanza Februari 23 hadi 25 mwaka huu, lakini Nyalandu alitumia usiku mmoja kukutana na kuzungumza na viongozi hao, moja baada ya mwingine, kisha kushiriki chakula cha jioni ambapo miongoni mwao walitoa hotuba za kumsifia (Nyalandu).
Hiyo inatajwa kuwa ni ziara ya kwanza kubwa kuwashirikisha viongozi wa dini,
huku taarifa za ndani kutoka vyanzo tofauti vikiihusisha na harakati za
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Nyalandu ambaye ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliotia nia ya kutaka kuteuliwa na chama hicho kugombea Urais, anahusishwa kuishawishi Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kuandaa ziara hiyo.
Vyanzo vya kuaminika, ziara ya viongozi hao inaweza kuwa sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushawishi wa nje ya chama (CCM) na kuongeza nguvu za uungwaji mkono ili ateuliwe kuwania nafasi hiyo.
Hata hivyo, ziara hiyo inaweza kumuweka kwenye mazingira magumu ya harakati za kutaka kuwania Urais, endapo itadhihirika kwamba ilikiuka kanuni za uteuzi wa mgombea Urais kupitia CCM.
Viongozi hao wa madhehebu tofauti walikuwa na walinzi, wapishi na wasaidizi binafsi na hivyo kufanya jumla ya watu walioshiriki ziara hiyo kukadiriwa kuwa 70, wakiwamo waandishi wa habari 10.
Walisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya kampuni ya Fastjet hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) walipowasili saa 5 usiku, Jumatatu iliyopita.
Mapokezi ya viongozi hao yaliongozwa na Afisa Uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete.
MAPOKEZI YA KIFAHARI
Baada ya mapokezi hayo, walitumia magari 12 ya kifahari aina ya Landcruiser yaliyokodiwa kutoka kampuni moja ya jijini Arusha na kwenda moja kwa moja hadi hifadhi ya Tarangire.
Mara baada ya kuingia katika hifadhi hiyo, viongozi hao walionyeshwa tembo na kupewa maelezo mbalimbali na waongoza watalii hadi walipofika katika hoteli ya Nyota tano ya Tarangire Sopa Lodge walipolala kwa siku tatu.
YALIYOJIRI
Viongozi hao waliandaliwa vyumba ambapo Askofu Mwingira na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim, walitumia vyumba vilivyokuwa vinafuatana na chumba alicholala Nyalandu. Haikujulikana mara moja sababu za kuwaweka viongozi hao karibu na Nyalandu.
Muda mfupi baada ya kukabidhiwa vyumba, viongozi hao wa dini walionekana wakimfuata Nyalandu kwa nyakati tofauti na kufanya naye mazungumzo ya faragha.
Tukio hilo lilifanyika awali kwa kuwashirikisha Nabii Ephata, Sheikh Salim na Askofu wa Kanisa la Anglikana, DayosisI ya Dar es Salaam, Dk. Valentino Mokiwa.
HAFLA
Viongozi hao walijumuika kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichohudhuriwa na Nyalandu, ambapo walizungumza huku wengi wao wakimsifia Waziri huyo kuwa ana sifa zinazomstahili kiongozi wa umma.
Pia, mdau mmoja wa utalii kutoka hoteli ya Tarangire Safari na askari wa wanyamapori hifadhini hapo, walielezea umuhimu wa uhifadhi na namna wanavyopambana na ujangili kwenye eneo hilo.
Pamoja na Nyalandu kutopatikana kuzungumzia tukio hilo tangu kumalizika kwa ziara husika, baadhi ya viongozi waliohusika katika ziara hiyo wameweka wazi yaliyojiri.
Jitihada za kumpata ofisini kwake zilishindikana na hata alipopigiwa kupitia simu zake mkononi, moja iliita pasipo kupokewa na nyingine haikupatikana.
Sheikh Salim, pamoja na mambo mengine alisifia jitihada zinazofanywa na kwenye sekta ya utalii kiasi cha kuongoza katika kuchangia pato la taifa.
Alisema ipo haja ya kuimarisha ulinzi na kuwadhibiti majangili wanaowaua wanyamapori hususan tembo na faru.
Alisema Nyalandu ni kiongozi bora aliyeonyesha dhamira safi katika kulinda wanyamapori nchini na kuwa miongoni mwa viongozi wanaotakiwa nchini.
Sheikh Salim alimshukuru Nyalandu kwa kuwapa fursa ya kushiriki ziara ya utalii wa ndani na posho kubwa, akisema, “tunashukuru sana kwani hata mifuko yetu imejaa.”
Kwa upande wake, mjumbe wa Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Alli Basaleh, alitumia vifungu vya Quran kuelezea namna kitabu hicho kinavyozungumzia uhifadhi na ulinzi wa wanyama pori.
Kiongozi mwingine, Nabii na Mtume Josephat Mwigira wa Kanisa la Efhata, (akimwangalia Nyalandu) alisema viongozi wa dini wameshaziona dalili za viongozi bora nchini, kauli iliyosababisha kupigiwa makosa.
VIONGOZI WANENA
Viongozi kadhaa walioshiriki ziara hiyo wamehojiwa na NIPASHE na kuelezea ‘ya mioyoni’ mwao lakini wakishindwa kuweka wazi kiasi cha fedha walicholipwa kama posho ya kujikimu.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, alisema ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha wajifunze kuhusu utalii wa ndani.
Alisema viongozi wa dini waliiomba ziara hiyo ya siku tatu na walitembelea Tarangire na hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Alipohojiwa kiasi cha fedha (posho) walicholipwa alicheka na kusema, “tulilipwa posho lakini fedha nyingi.”
Sehemu ya mahojiano ilikuwa hivi:
Swali: Kuna taarifa kuwa mmelipwa kiasi kikubwa cha posho, unaweza kuweka wazi ni Shilingi ngapi?
Jibu : Sio kweli kwamba ni fedha nyingi. Tumelipwa posho ya kawaida tu.
Swali: Inakuwaje mlipwe posho wakati umesema ziara hiyo mliiomba wenyewe ili mshiriki utalii wa ndani?
Jibu: Si unajua tuliziacha familia zetu.
Kwa upande wake Mchungaji Alphonce Temba wa Kanisa la Penuel Healing ministry la jijini Dar es Salaam, alisema ziara hiyo ilitokana na maombi ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini.
Alisema lengo la ziara hiyo ililenga kujifunza masuala yanayohusiana na kushamiri kwa ujangili na biashara ya meno ya tembo, ili wawe katika nafasi nzuri ya kuwahamasisha wananchi kukabiliana na changamoto hiyo.
Alimsifu Nyalandu kwa kufanikisha ziara hiyo na kuwashangaa watu wanaompinga waziri huyo.
Temba, alisema viongozi hao wanatarajia kufanya ziara nyingine pembezoni mwa mbuga na hifadhi za taifa, lakini hakusema itafadhiliwa na nani. “Waziri amekuja na kitu kipya, nashangaa ni kwa nini wanampiga vita. Siyo kwamba haya anayoyafanya ni masuala ya Urais sisi hatujapewa dokezo lolote kuhusu Urais,” alisema.
Alisema katika utalii huo jambo jingine aliloliona ni kwamba kampuni za utalii zimekuwa zikijipatia fedha nyingi huku wabunge wengine wakiwa wanufaika wa kadhia hiyo.

Chanzo: Nipashe
No comments:
Post a Comment