Fundi Samweli na Saraha enzi za
penzi lao
|
Staa wa muziki Saraha, amefunguka kwa mara ya
kwanza kabisa tangu kuvunjika kwa mahusiano yake na mtayarishaji muziki maarufu
Fundi Samweli'
kupitia mahojiano yake na eNewz
ameeleza kuwa mapenzi sio suala rahisi
na kusisitiza kuwa hakuna shida yoyote
kubwa iliyosababisha kutengana kwao.
Saraha ameieleza eNewz kuwa, safari
yao ya mahusiano ilifikia mahali ambapo kila mmoja aliona kuna umuhimu wa
kuchukua njia yake tofauti, huku akisisitiza kuwa kwa sasa, mpenzi wake mkubwa
ni muziki tu ambao yupo nao wakati wote.
Saraha amesema kuwa, anajipanga kwa ajili ya kurejea
nchini ndani ya miezi kadhaa kwa ajili ya upigaji picha za video yake mpya
katika kuthibitishia mashabiki kuwa muziki, hususan ule wa Bongo Flava ndio
mpenzi wake mkubwa sasa.
No comments:
Post a Comment