Watu 41 wamefariki katika eneo la Changarawe, Mafinga
mkoani Iringa,nyanda za juu kusini mwa Tanzania, baada ya basi la kampuni ya
Majinja Express walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na Lori.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mvungi
amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya hao 41 waliopoteza
maisha,wanaume ni 33,wanawake watano na watoto watatu.
Akielezea chanzo cha ajali hiyo, Kamanda Mvungi amesema
kuwa dereva wa Lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara swala
lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo
na kusababisha kugongana uso kwa uso.
Hata hivyo kasha la lori hilo liliangukia basi hilo la
kampuni ya Majinja na kusababisha vifo kwa abiria hao.
Miili ya waliofariki katika ajali hiyo imehifadhiwa
katika hospitali ya Mafinga mkoani humo,na majeruhi wanaendelea kupatiwa
matibabu katika hospitali hiyo.
Kwa mjibu wa kamanda mvungi taarifa zaidi zitaendelea
kutolewa kuhusiana na ajali hiyo.
Kumekuwa na ajali za mara kwa mara za barabarani katika
nchi za Afrika mashariki ambazo husababishwa na mwendo wa kasi wa madereva na
ubovu wa barabara. CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment