Askofu mkuu mstaafu wa mji wa Capetown na mshindi wa tuzo
la Nobel Desmond Tutu pamoja na mkewe wamemshtaki na mashtaka ya uhalifu mjukuu
wao.
Katika taarifa kupitia wakfu wa Desmond na Leah Tutu
hawakutoa maelezo zaidi ,lakini maafisa wa polisi wa Afrika kusini wamesema
kuwa wanachunguza kesi kuhusu uharibifu wa mali kwa makusudi.
Mjukuu huyo Ziyanda Palesa Tutu anatarajiwa kujisalimisha
kwa polisi.
Amesema kuwa amehuzunishwa sana.
Wakfu huo umesema kuwa familia imeshangazwa na kitendo
hicho na wanatumai kwamba wataliweka nyuma swala hilo hivi karibuni.
BBC
No comments:
Post a Comment