Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amejerea nyumbani
hapo jana, baada ya kuwepo kwa jaribio la kumpindua akiwa nchini Tanzania
kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokuwa
wakijadili mgogoro wa Burundi.
Maafisa wa serikali wanasema kurejea nyumbani kwa Rais
huyo sasa ni ishara kuwa jaribio la kumpindua limeshindikana.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Niyongabo
amesema vikosi vya serikali ya Burundi vimefanikiwa kudhibiti hali ya mambo na
kuzima jaribio la kumpindua Rais Pierre Nkurunziza.
Tayari vikosi vya serikali vimetia nguvuni baadhi ya
wanajeshi waliokuwa wakijaribu kuipundua serikali huku baadhi yao wakijitetea
kuwa walirubuniwa.
Hapo jana kulikuwa na mapigano makali karibu na radio ya
taifa kati ya majeshi yaliyojaribu kuipindua serikali na yale yanayomtii Rais
Pierre Nkuruziza.
BBC
No comments:
Post a Comment