BAADA ya mashabiki wake kumtaka aongeze mtoto wa tatu,
msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shaban (Keisha), ameibuka na kuweka wazi kwamba
hana mpango wa kuzaa tena kwa sasa.
Keisha aliliambia MTANZANIA kuwa, sababu kubwa
inayomfanya asitamani kuongeza mtoto kwa sasa ni kutokana na kuwa na watoto
wawili wa kiume wenye umri mdogo.
“Najua watu wengi wanapenda watoto na hata mashabiki
wangu wanatamani sana niendelee kuzaa, kiukweli bado nahitaji kulea madume
yangu, kwani umri wao bado ni mdogo sana,” alisema Keisha.
Mtoto wa kwanza wa msanii huyo ana miaka minne na wa pili
ana mwaka mmoja.
“Kama nitabeba ujauzito mwingine kwa sasa mimi na baba
yao tutakuwa hatuwatendei haki hawa watoto wetu, wanahitaji muda wa kukua zaidi
ndipo tufikirie kuongeza wenzao wengine,” alisema Keisha.
No comments:
Post a Comment