MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Wema Sepetu, amedai kwamba
itabaki kuwa siri yake kama ni kweli anamiliki bastola ama la kwa kuwa si sifa
kutangaza umiliki wa silaha.
“Hii ni siri yangu kama namiliki bastola au la, lakini
mimi sioni ajabu kumiliki bastola, mtu kama mimi mwenye maadui wengi inasaidia
katika ulinzi wa maisha yangu,” alieleza Wema.
Wema aliendelea kuwataka wanaojiuliza kama anamiliki
bastola ama la waendelee na mambo yao mengine kwa kuwa hawatajua jambo hilo
ambalo ni siri katika kuimarisha ulinzi wake.
MTANZANIA
No comments:
Post a Comment