Polisi mkoani Simiyu inamshikilia mkazi wa Kijiji cha
Bukigi, Kata ya Malampaka wilayani Maswa, kwa tuhuma za kukutwa na viungo
vinavyosadikiwa kuwa ni vya binadamu likiwamo fuvu la kichwa.
Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji hicho
na mganga wa kienyeji, alikamatwa nyumbani kwake baada ya kuwapo kwa taarifa
kuwa alikuwa amewahifadhi majambazi ili awazindike.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi alisema
jana kuwa mwenyekiti huyo alikamatwa Mei 9, kijijini hapo baada ya kupata
taarifa ya kuwapo majambazi nyumbani kwa mwenyekiti huyo. Alisema baada ya
taarifa hizo, polisi walifanya msako nyumbani kwa mwenyekiti huyo na kufanikiwa
kukamata vitu hivyo.
Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kama
viungo hivyo ni vya binadamu na kama anahusika navyo, kwa sababu vilikutwa nje
ya nyumba yake.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment