waziri aliyeuawa |
Idara ya ujasusi ya Korea Kusini imesema kuwa waziri wa
ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi
hiyo, Kim Jong-un.
Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol
alikutana na mauti yake baada ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele
ya mamia ya maafisa wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi Aprili.
Bwana Hyon anasemekana kuwa alisinzia katika hafla
iliyokuwa ikihutubiwa na rais Kim jambo lililomuudhi sana kiongozi huyo wa
kiimla.
Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na
usiri wa serikali ya Korea Kaskazini.
Waziri wa ulinzi wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa
muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
Bwana Hyon alipandishwa cheo na kuwa Generali mwaka wa
2010 na kuuawa kwake kunatia shaka udhabiti wa uongozi wa rai Kim Jong -un.
Hyon alipandishwa cheo na kutangazwa kuwa waziri wa
usalama wa taifa mwaka uliopita.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Seoul anasema mauaji hayo
ya kikatili mbele ya umma ikiwa yatathibitishwa, yanaonyesha athari za uasi
dhidi ya Kim Jong-un.
Mapema idara hiyo ya ujasusi ilisema viongozi wakuu
katika serikali ya Korea Kaskazini wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa
katika eneo la hadhara alikouawa
Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa korea kaskazini
kuamrisha kuuawa kwa kiongozi mkuu serikalini ilikuwa ni mwaka wa 2013
alipoamrisha ami wake
Chang Song-thaek - kukamatwa na kutiwa kitanzi.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa
katika eneo la hadhara alikouawa mbele ya umma.
No comments:
Post a Comment