Mshangao! Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo,
marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa
ili azae, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya
kaburi.
Hayo yanakuja siku chache baada ya
Wema aliyewahi kuwa
mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo
mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.…
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.
Waandishi wetu
Mshangao! Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo,
marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa
ili azae, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya
kaburi.
Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa
mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo
mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.
Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu
Steven Kanumba ‘The Great’, Charles Kusekwa Kanumba.
Akizungumza na waandishi wetu, baba huyo alisema kama
kweli Wema alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao
ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto) hivyo anatakiwa
kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba ambaye ni bibi wa
babu wa mzee Kanumba.
Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na
ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).
“Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili, moja ni
kufariki dunia au ‘kujikila’ (kujilaani) kwa kutokuzaa, pengine ndicho
kilichomtokea Wema,’’ alisema baba Kanumba.
KUTAMBIKA KABURINI
Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo alishafariki dunia
kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda kaburini kwake kufanya
tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kiasili na mikononi wameshika
vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema kukaza moyo.Alisema kuwa wakiwa kaburini
hapo, Wema alitakiwa achotewe mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya
kuomba msamaha kwa kilichotokea.
VITU VYA TAMBIKO
Alisema walitakiwa waende na maziwa, unga wa mtama na
hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.
KURITHIWA NA NDUGU
Aliendelea kudadavua kwamba, kwa sasa Kanumba hayupo
duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa damu kwenda
kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua mlango wa kizazi, hata
kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.
MAMA MKUBWA NI NANI?
Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni bibi yake mzee
Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa wanawake walioshindwa
kupata watoto au wenye tatizo la kizazi.
Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa,
ingekuwa zamani ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa
vikali.Gazeti hili lilipomtafuta Wema ili kumfikishia taarifa hizo hakupatikana
hivyo jitihada zinaendelea.
GPL
No comments:
Post a Comment