Wazazi wanapotengana watoto wanaathirika, wasameheane tu warudiane.
MUIMBAJI
wa muziki wa Injili, Flora Mbasha amesema yupo tayari kurudiana na mume wake
Emmanuel Mbasha, ikiwa atakwenda kumuangukia miguuni na kumuomba msamaha.
Flora
alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa
ushahidi wake juu ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mbasha ambayo inasikilizwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
“Mbasha
nimemsamehe siku nyingi na nipo tayari kuishi naye iwapo atakuja kuniangukia
miguuni na kuniomba msamaha… lakini hili (ubakaji) ni suala la mahakama,”
alisema.
Alipoulizwa
baba halali wa mtoto wake wa kike aliyejifungua hivi karibuni, alisema hawezi
kulizungumzia jambo hilo hivi sasa.
“Siwezi
kulizungumzia nikifanya hivyo nitakuwa simtendei haki mwanangu. Siwezi kubadili
mitizamo ya watu jinsi wanavyotafakari kuhusu jambo hili,” alisema.
Wakili
wa Serikali, Nassoro Katuga alisema awali Flora alitoa ushahidi wake mbele ya
Hakimu Flora Mjaya na kueleza alivyosimuliwa na binti huyo anayedai kubakwa na
Mbasha.
Katuga
alikuwa akitoa ufafanuzi huo kwa waandishi kwa vile kesi hiyo inasikilizwa
katika mahakamani ya siri kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai
ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu ili kulinda
haki ya binti huyo.
Wakili
alisema Flora aliieleza Mahakama kuwa Mei 23 mwaka jana, alimkuta binti huyo
akiwa mnyonge huku amelala kitandani na kujifunika shuka.
Alisema
alimhoji binti huyo kama alikuwa anaumwa au la lakini hakumjibu chochote.
Flora alisema siku iliyofuata Mei 24, waliondoka na kwenda kanisani yeye na watoto waliokuwapo nyumbani lakini Mbasha hakuongozana nao.
Flora alisema siku iliyofuata Mei 24, waliondoka na kwenda kanisani yeye na watoto waliokuwapo nyumbani lakini Mbasha hakuongozana nao.
“Flora
alipotoka kanisani na watoto aliwarudisha nyumbani kisha akaondoka na kwenda
hotelini kwa sababu alikuwa na ‘stress’ (mawazo) lakini akiwa huko alipigiwa
simu na mdogo wake Suzan (shahidi wa pili) akimueleza kile alichoambiwa na
binti huyo,” alisema Katuga.
Alisema
Flora baada ya kuambiwa jambo hilo kwa simu alimwambia mdogo wake huyo ampeleke
binti huyo katika hoteli iliyoko Sinza.
Alisema
walipofika binti huyo alimsimulia tukio hilo la kubakwa na ndipo akawaambia
waende wakatoe taarifa hizo kituo cha polisi kabla ya kwenda hospitalini.
Mahakama
hiyo ilisikiliza ushahidi wa Flora kwa takriban saa nne.
Awali
wapiga picha walizuiliwa na ndugu zake kumpiga picha huku wakidai kuwa
watawashtaki.
“Mnataka kumpiga picha za nini, mmetumwa… mnajua sheria za nchi nyinyi,” alisikika mmoja wa ndugu zake.
“Mnataka kumpiga picha za nini, mmetumwa… mnajua sheria za nchi nyinyi,” alisikika mmoja wa ndugu zake.
Tukio
hilo lilizua minong’ono mingi kutoka kwa wananchi waliofika mahakamani hapo
kufuatilia kesi mbalimbali.
“Jamani
kwani hawa si wapiga picha… waandishi si wanaruhusiwa kuchukua matukio na
kwenda kuyaripoti kulikoni hawa wazuiliwe…jambo hili linashangaza kweli kweli,”
alisema mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Tukio
hilo lilimshangaza pia Wakili George Mwalali aliyekuwa mahakamani hapo ambaye
alisema kitendo hicho ni kosa.
“Haiwezekani
mzuiliwe kupiga picha mpo sahihi kwa sababu hapa ni nje ya Mahakama, nitakwenda
kuzungumza na wakili mwenzangu juu ya jambo hili,” alisema.
Baadaye
ndugu hao wa Flora waliwafuata waandishi na kuwauliza kwa nini walikuwa
wakipiga picha hizo na kudai kuwa walikuwa wakiwazuia kwa vile walipata taarifa
kwamba kuna mtu amewapa fedha wapige picha hizo.
“Hapana
ndugu yangu, sisi hakuna aliyetupatia fedha… tunachotaka ni habari hii na si
vinginevyo,” alisema mmoja wa wapiga picha.
Mmoja
wa ndugu hao alisema kilichokuwa kikiwaogopesha na kuamua kuzuia utekelezaji wa
hatua hiyo ni kitendo cha baadhi ya waandishi kuweka kwenye mitandao ya jamii
habari ambazo si sahihi.
“Kwa
mfano zile picha zilizosambazwa mwanzoni zilitushangaza kwani si za huyu binti
aliyebakwa, sijui walizitoa wapi, huko ni kuchafuliana majina,” alisema.
Baada
ya ndugu hao kuridhishwa na ufafanuzi waliopewa na wapiga picha waliokuwa
mahakamani hapo waliwaruhusu kuendelea na kazi yao.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi April 16 mwaka huu itakapotajwa tena. CHANZO MTANZANIA
Kesi hiyo iliahirishwa hadi April 16 mwaka huu itakapotajwa tena. CHANZO MTANZANIA
No comments:
Post a Comment