Hapo mwisho wa hii habari kuna sehemu wamesema wameweka kikosi maalumu kitakachoshughulikia masuala ya watu wanaozunguka zunguka nje za ofisi za watu pasipo shughuli maalumu.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
linamshikilia mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, Haroub Mtopa (44) kwa kujifanya
mtumishi wa umma kupitia cheo cha Katibu wa Rais, Jakaya Kikwete, Prosper
Mbena.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema
mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi jioni.
Kova alisema Mtopa alikuwa na mazoea ya
kujifanya mtumishi wa Ikulu kwa nia ya kudanganya watu kwamba anaweza
kuwasaidia shida zao ili ajipatie fedha.
Katika kufanya kazi zake za kitapeli, Kova
alisema mtuhumiwa huyo alikuwa akiingia na kutoka Ikulu mara kwa mara, huku
akijifanya kuwa na shida nyingi hivyo alikuwa akiomba msaada.
‘’Huyu mtu ni tapeli wa muda mrefu sana,
tulimkamata baada ya mwananchi mmoja kuzungumza na mtuhumiwa huyo na kuahidiana
kumpa Sh 500,000 na kutanguliziwa Sh 250,000.
Baadae aliitwa siku nyingine afuate fedha
iliyobaki. ‘’Mwananchi huyo ambaye hakumtaja jina, alimhofia Mtopa ndipo
alipotoa taarifa Polisi kisha akamwambia mtuhumiwa huyo aende kuchukua fedha
iliyobaki, hatua iliyosaidia Polisi kumkamata kwa urahisi,’’ alisema.
Kova alisema kuwa mtu huyo ni hatari kwa sababu
kutumia cheo cha Katibu wa Rais wakati inamaanisha kwamba mtu huyo aliweza
kutapeli watu wengi sana kupitia cheo hicho.
Kwa mujibu wa Kova, mtuhumiwa huyo amekuwa
akizunguka katika wizara mbalimbali ikiwamo ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wizara ya Maji na taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii, kwa
lengo la kuomba msaada.
Alisema kabla ya kumkamata, walishirikiana na
Ikulu baada ya watu wengi kupeleka malalamiko yao kuhusu mtuhumiwa
huyo.
Kova aliwaasa wananchi kuepuka kujifanya
watumishi wa umma kwani ni kosa kisheria na kuongeza kuwa wameweka kikosi
maalumu kitakachoshughulikia masuala ya watu wanaozunguka zunguka nje za ofisi
za watu pasipo shughuli maalumu.
CHANZO HABARI LEO
No comments:
Post a Comment