Bafu linaweza kuwa ndicho chumba kigumu zaidi kusafisha. Kufanya kazi
moja kwa hatua itakusaidia kumaliza bafu zima fasta. Hizi ni hatua tano za kufanya
kila mahali pawe safi bafuni.
Hatua ya 1: Weka dawa za
kusafishia zile sehemu sugu, kwa mfano nyunyiza vim kwenye taili zenye ukurutu
Hatua ya 2: Safisha sinki na kioo
Hatua ya 3: Safisha choo
Hatua ya 4: Safisha shower na tub
Hatua ya 5: Safisha sakafu na mwaga taka
Vifaa unavyohitaji
Dekio/mopper + ndoo
Sponji
Brushi ya kusugulia kwenye taili
Brashi ya kusugulia kwenye bakuli la choo
Kitaulo kikavu cha kufutia
Sabuni na dawa za kusafishia bafuni
Dawa ya kusafishia kioo
Na of course maji.
Kuna ambacho nimesahau labda?
Hongera! Umeweza kumaliza kusafisha bafuni fasta, nenda
kanywe juisi ama lala kidogo! Unastahili!
No comments:
Post a Comment