Mchezaji
wa timu ya taifa ya England ambaye pia anakipiga katika klabu ya soka
Sunderland Adam Johnson amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya
mapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.
Polisi katika eneo la
Durham wamesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekamatwa mapema
wiki hii kwa tuhuma za kufanya ngono na binti mwenye umri wa chini ya
miaka 16, na amebaki chini ya ulinzi. Taarifa ndani ya klabu yake
zinasema kuwa mchezaji huyo amesimamishwa kusubiri matokeo ya uchunguzi
wa polisi.
Taarifa za kukamatwa kwake zilitolewa mapema kupitia gazeti
la The Sun. Kukamatwa kwake kunakuja muda mfupi kabla hajasafiri na timu
yake ya Sunderland kwenda kukutana na Hull kwa michezo ya Ligi kuu ya
England iliyopangwa kuchezwa leo usiku. Sunderland imesema haitaendelea
kuzungumzia kukamatwa kwa mchezaji wake.
No comments:
Post a Comment