Sheria ya mtandao huu wa kijamii inasema ''Marufuku
kuchapisha picha au video chafu zilizopigwa au kurekodiwa kisha kusambazwa bila
ridhaa ya muhusika aliye kwenye video na picha hizo''
Msemaji wa Kampuni ya Twitter amesema watumiaji
watakaobainika kukiuka masharti mapya ''Anuani zao zitafungiwa''
Watumiaji wanaopeleka malalamishi Twitter kuhusu picha na
Video zilizochapishwa watatakiwa kujitambulisha na kuithibitishia Kampuni kuwa
hawakuwahi kutoa idhini ili kuchapisha picha au video mtandaoni na kuonekana
kwa hadhira.
Yeyote atakayebainika kuchapisha picha hizo kinyuma na utaratibu wa sheria hii mpya atatakiwa kufuta kwanza kabla ya kurejeshwa tena mtandaoni.
Nchini Uingereza na Wales imeweka sheria ambayo mtuhumiwa
atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka miwili gerezani.
Sheria hiyo inagusa picha zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii na Ujumbe mfupi.
Majimbo kadhaa ya Marekani wameweka Sheria ya kupambana
na vitendo hivi hasa California,Texas na Utah.
Mabadiliko haya ya twitter yamekuja baada ya Kampuni hiyo kukosolewa kuwa imekuwa haifanyi jitihada madhubuti dhidi ya matumizi mabaya ya mtandao unaofanywa na watumiaji wake. CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment