WANAFUNZI wawili wa darasa la pili katika Shule ya Msingi
Ongoma iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamekutwa wakilawitiana
katika shamba la migomba jirani na shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,
Jerad Kesi, aliiambia MTANZANIA jana kwamba tukio hilo lilitokea Machi5 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo,
Mwalimu Kesi alisema mmoja wa wazazi wa watoto hao alivamia shuleni hapo na
kuwapiga walimu kwa kile alichosema kuwa walimu hao walikuwa wamemdhalilisha
mtoto wake.
“Siku ya tukio, wanafunzi
wawili wa darasa la pili na mmoja wa darasa la kwanza walikutwa na mwalimu
wangu wakilawitiana kwenye migomba.
“Walipojua mwalimu amewaona,
walikimbia na kuacha nguo zao pamoja na yule wa darasa la kwanza. Tulipomhoji
yule mtoto aliyebaki alikubali kwamba amekuwa akilawitiwa na kwamba ameshafanyiwa
kitendo hicho kama mara saba hivi,” alisema Mwalimu Kesi.
Baada ya wanafunzi hao kutimua
mbio, Mwalimu Kesi alisema walirudi nyumbani na baadaye mmoja wa wazazi wao
alifika shuleni hapo na kuwashutumu walimu hao kwamba wamemdhalilisha mtoto
wake kwa kumvua nguo.
“Baada ya majibizano kati ya
walimu na mzazi huyo, mzazi huyo aliwapiga walimu kwa fimbo na kuwajeruhi.
“Kwa hiyo, nilichokifanya
nilikwenda kutoa taarifa polisi na kupewa RB namba MJ/RB/988/15 kwa ajili ya
kumkamata mzazi huyo,” alisema mwalimu huyo.
Naye Mwalimu Idda Kilawe
ambaye ndiye aliyewakuta
wanafunzi hao wakilawitiana, aliiambia MTANZANIA, kwamba siku ya tukio aliwakuta wanafunzi hao wakiwa ndani ya kibanda walichokuwa wamekijenga kwenye migomba.
wanafunzi hao wakilawitiana, aliiambia MTANZANIA, kwamba siku ya tukio aliwakuta wanafunzi hao wakiwa ndani ya kibanda walichokuwa wamekijenga kwenye migomba.
“Niliwakuta wakiwa wamejenga
kibanda cha miti na kukiezeka kwa matawi ya miti na ndani yake walikuwa
wanafunzi watatu na wawili kati yao ndiyo walikuwa wakilawitiana.
“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa
natoka kuchukua matokeo ya mitihani na nilipokaribia eneo la tukio, nikasikia
sauti za watoto. Niliposogelea eneo hilo niliwaona wanafunzi wawili wakiwa uchi
na yule mdogo ndiye alikuwa amevaa sare. waliponisikia, wakakimbia,” alisema
mwalimu Kilawe.
Mratibu wa Elimu, Kata ya Uru Kaskazini, Monyaichi Lyimo, alisema amekwisha
kupata taarifa za tukio hilo.
No comments:
Post a Comment