Leo tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo
Kikuu cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe
29/03/2015.
Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na
risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.
Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:
Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha
kwamba silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima. Kuhusu
risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki Bunduki aina ya Short
Gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina ya hizo zilizokamatwa.
Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu
Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao pia wanahojiwa
kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi zilizotajwa hapo juu wakati wao sio
wamiliki halali za silaha hiyo na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa
sheria.
Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi
litapelekwa kwa mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,S. H. KOVA,DAR ES SALAAM.