Mahakama nchini Ivory Coast imemhukumu aliyekuwa mke wa
Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani.
Simone
Gbagbo amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika
ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011.
Simone
Gbagbo alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, aliyekuwa rais wa nchi hiyo
Laurent Gbagbo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu
katika mahakama ya uhalifu mjini The Hague Uholanzi.
Katika
ghasia hizo watu takriban elfu tatu walifariki dunia. CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment