CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaomba Watanzania kumpuuza
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Slaa
kwa madai aliyoyatoa ya kuwepo kwa njama za kutaka kuuawa na viongozi wa juu wa
CCM kwa vile
madai hayo ni ya uongo.
madai hayo ni ya uongo.
CCM imetoa rai hiyo kwa Watanzania huku ikisema
hatua yake hiyo haijalenga kuingilia utaratibu na sheria kwa vyombo vya
serikali kufuatilia madai hayo iliyoyaita ni ya uongo na ambayo amekuwa
akiyatoa mara kwa mara.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
ilisema tuhuma zilizotolewa na Dk Slaa kupitia kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema Mabere Marando ni za kipuuzi, lakini pia ni za uongo.
“Machi 8, mwaka huu, Dk Slaa, Katibu Mkuu wa
Chadema kupitia kwa Marando alitoa tuhuma kwa Serikali na kuwahusisha baadhi ya
viongozi wa juu wa CCM kuwa wanapanga njama za kumdhuru Katibu Mkuu huyo wa
Chadema.“Kimsingi tuhuma hizi ni za kipuuzi, lakini uongo huu usipojibiwa
unaweza kugeuzwa kuwa ajenda na chama hiki cha Chadema kwa kukosa ajenda
zingine za maana.
“Hakuna asiyejua kuwa Chadema kwa sasa
kinapumulia mashine, hivyo maneno na matendo yao kwa sasa lazima yalenge
kujaribu kujinasua na balaa la kufa kwa chama hicho.“Ni vizuri Watanzania
wakakumbuka historia ya tuhuma lukuki zilizowahi kutolewa na Katibu Mkuu huyu
wa Chadema tangu aanze siasa na ambazo zote zilikujathibitika kuwa ni za
uongo,” alisema Nape katika taarifa hiyo ya CCM.
Akitolea mfano Nape alisema akiwa Singida katika
kampeni za urais za mwaka 2010, Dk Slaa aliwatangazia wananchi mkutano kwamba
kulikuwa kumekamatwa lori kubwa la mizigo lililojaza karatasi za kura za urais
zilizokuwa tayari amepigiwa kabisa mgombea urais wa CCM, Dk Jakaya Kikwete.
“Katika kuonesha kwamba alikuwa na
uhakika wa jambo hilo, alisema hadi namba za lori hilo na tela lake kisha
akasema lilikamatwa katika mji wa Tunduma, Mkoa wa Mbeya wakati likiingia
kutoka Lusaka Zambia. Lakini Polisi baada ya kulikamata na kulipekua hadharani
lilikutwa na shehena ya vipodozi vya akina mama na manukato.” CHANZO: HABARI LEO
No comments:
Post a Comment