Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego hivi karibuni aliweka
wazi majibu yake baada ya kupima UKIMWI kupitia account yake ya Instagram na
kwamba alikuwa yupo safi yaani(Negative).
Alipoulizwa sababu ya kupima ngoma
alisema kuwa alikuwa akiumwa ugonjwa wa Malaria na alikuwa hajaugua kwa muda
mrefu na alipokwenda hospitali ilibidi apime na ngoma ingawa ni kawaida yake
kupima mara kwa mara.
‘’Nilipima baada ya kuumwa Malaria lakini huwa ni kawaida
ya kupima ngoma hata mke wangu(Siwema) alipokuwa mjamzito tulikwenda pamoja
kupima hospitali,’alisema Nay. Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke
wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo
ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.
‘Unajua ni mambo ya ujana ni kweli nilishawahi kuchepuka
lakini siwezi kusema ni mara ngapi si unajua mama watoto anaweza kukasirika?
Lakini nilikuwa makini sana na namwomba sana msamaha mke wangu na sitegemei
kuchepuka tena,’’alisema Nay.
No comments:
Post a Comment