Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, (pichani),
ametoa siku saba kwa Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam, kuhakikisha inajenga
mtaro wa kupitisha maji machafu ili kuondokana na majitaka hayo kuingia kwenye
mitaro mipya inayojengwa.
Makonda alitoa kauli hiyo alipotembelea kwenye maeneo ya
Mikocheni kukagua miundombinu ya barabara na mitaro inayojengwa ili kudhibiti
athari za mvua zinazotarajia kunyesha wakati wowote.
Makonda, alishuhudia mtaro wa majitaka ya hospitali hiyo
ukitiririsha uchafu kuelekea kwenye mitaro mipya inayojengwa hali
iliyosababisha mitaro hiyo kujaa taka kabla ya kukamilika kwake.
Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Mbaraka Mkwiya, alisema
miradi ya ujenzi wa mitaro ya maji taka kwenye bonde la mpunga unagharimu
takribani Sh. bilioni sita na barabara tano za mitaa ya Mikocheni na
Msasani ambazo zitagharimu Sh. bilioni 3.3 ambayo yote, inatarajia
kukamilika miezi michache ijayo.
CHANZO NIPASHE
No comments:
Post a Comment