Waziri mkuu nchini Morocco Abdelilah Benkirane ameamrisha
kufanywa uchunguzi kuhusu matangazo ya runinga ya tamasha ya mwanamuziki
Jennifer Lopez.
Tamasha hiyo inayofahamika kama Mawazine iliandaliwa
mjini Rabat tarehe 29 mwezi Mei na kupeperushwa na kituo cha runinga cha 2M.
Bwana Benkirane amesema picha kutoka kwa tamasha hilo
zilikuwa potovu na kuongeza kuwa matangazo hayo yalikiuka sheria za matangazo
ya picha za nchi hiyo.
Wiki iliyopita waziri wa mawasiliano nchini Morocco
alilaumiwa kwa kuruhusu tamasha hilo kupeperuswa kupitia runinga ya taifa hali
iliyobabisha kuwepo wito wa kumtaka ajiuzulu.
Akimuandikia barua rais wa halmashauri ya matangazo ya
redio na runinga nchini Morocco , bwana Benkirane alitaka halmashauri hiyo
kuwachukulia hatua za kisheria wale waliohusika.
Alisema kuwa wale wanaosimamia shirika hilo la utangazaji
walishindwa kuingilia kati na kuzuia kutangazwa kwa picha potovu.
Lopez
amefanya tamasha nchini Morocco awali bila kuwepo tatizo lolote , lakini hii
ndiyo mara ya kwanza moja ya tamasha zake zimepeperushwa kwa njia ya runinga.
Nalo kundi linalohusika na elimu la TMZ linasema kuwa
linamshtaki mwimbaji huyo kwa kuwa Lopez ameshusha hadhi ya wanawake.
BBC
No comments:
Post a Comment