Susu
ya mvinyo ni njia rahisi na ya gharama nafuu kabisa ya kuhifadhi chupa za mivinyo
na wakati huohuo zikiweka mivinyo yako katika muonekano wa kimapambo. Susu hizi
ni kwa ajili ya muonekano ila sio kwamba zinakuja na jokofu hapana. Katika
kuandaa makala hii nimefanya mazungumzo na Jack ambaye ni mtaalam wa kuhifadhi
mvinyo na afisa mauzo katika duka la mivinyo. Anasema kuwa kama wewe
huna
shauku ya kunywa mvinyo haraka haraka na kuumaliza huna haja ya kuhifadhi
mvinyo wako kwenye jokofu. Susu ya kuhifadhia mivinyo ni kwa wale watumiaji na
wakusanyaji wa mivinyo bila kujali muda au kipindi na hivyo wanapendelea kuwa
na hifadhi ya mivinyo mbalimbali muda wote nyumbani kadri wanavyoipata.
“Kwa
lengo lolote kama wewe ni mtu wa kukusanya mivinyo na unaenda kuitumia polepole
nyumbani, haiharibiki pale inapokuwa imehifadhiwa kwenye susu yake ndani ya
miaka mitatu hadi mitano,” anasema Jack.
Kuwa
na eneo la kuhifadhi mivinyo kwenye nyumba yako inasikika vizuri, na kwa maana
hiyo hutajali kuwa na susu ya kuihifadhia. Kimsingi susu za kuhifadhia mivinyo
ni kwa wale wanaofurahia kuwa na mivinyo kila wakati nyumbani, anasema Jack. Kwa
hawa wanaopenda kunywa mvinyo wakati wowote watakapo, susu ya mvinyo sio tuu
itasaidia kufanya kaunta ziwe safi, yaani kutorundikana hizo chupa, lakini pia
kufanya muonekano wa kuvutia hapo mahali utakapoamua kuweka susu yako, iwe ni
jikoni, sebuleni au chumba cha chakula. Na wakati huo huo kuzuia ajali ya chupa
kugongana na kuvunjika
“Eneo
lenye susu za mvinyo limekuwa kitovu cha jicho kwenye nyumba za wapenda mvinyo,”
anasema Jack. Na unapoamua kuburudika au kuburudisha nyumbani usitanie, zile
nyakati za kuwa na kisusu cha mivinyo kidogo ndani ya kabati la sebuleni
zinaishia. Sasa kuna susu za kusimama peke yake na ambazo zinatengenezwa kama
pambo la ndani vilevile, kama hupendi mambo haya huwezi kuelewa. Na pia kuna
zile ndogo za kuweka juu ya kaunta au meza.
Jack
anasema kama unataka susu ya mivinyo yenye vigezo vyako ni vyema
ukatengenezesha. Kutoa oda ya susu ya namna hii itasaidia kupata mtindo ule
unaotaka na wa kuweza kuenea kwenye eneo unalotaka kuiweka; wakati ambapo zile
zilizotengenezwa tayari zinapatikana kwenye vipimo maalum tu.
Kwenye
kuchagua susu za mvinyo kuna aina nyingi. Zipo za maumbo mbalimbali na pia
zenye visehemu vya kutumbukiza chupa kwa uwingi mbalimbali, hivyo hutabanwa na
aina na mtindo wa susu unayotaka.
Kwa ajili susu za mivinyo zinatumika kuhifadhi mivinyo
kwa miaka mitatu hadi mitano baada ya kuinunua, kuamua ni ukubwa gani unahitaji
ni lazima ujue ni mivinyo mingapi utanunua/utakunywa kwenye kipindi hicho, hivyo unaweza
kukisia ni chupa ngapi za mivinyo utahifadhi kwenye susu yako. Je susu yako utaiweka
juu ya meza, kaunta, unaitundika ukutani ama inasimama peke yake.
Susu za mvinyo zimetengenewa kwa malighafi mbalimbali kama vile chuma cheusi, chuma cha
silva, mbao zilizopakwa rangi na mbao zilizoachwa asilia bila rangi. Ni ipi
unapenda? Susu inayopendeza ni ile ambayo kila chupa ina kisehemu chake cha
kuhifadhiwa.
Kuna vitu vinavyoambatana na susu za mvinyo, kama
vile kimeza, sehemu ya kutundikia glasi za kunywea, droo au shelfu. Fikiria kama utavihitaji
pamoja na susu yako.
Sasa,
kumbuka kuwa susu za mvinyo zinauweka mvinyi kwenye joto la chumba susu ilipo,
kwa ajili tumeshasema hii susu haina jokofu. Hii ina maana mvinyo wako unaweza
kuwa na hali ya uchungu baada ya miaka mitatu hadi mitano –hii haina maana kuwa
utashindwa kuunywa. Ila sasa baada ya hapo unatakiwa kufikiria mara mbili kabla ya kuuweka kwenye
jokofu. Nilipokuwa na Jack nimemuuliza kuwa kama hilo ni wazo zuri ama laa.
Jack ametoa changamoto hii kwa suala la kuweka
mvinyo kwenye jokofu.
“Kuweka
mvinyo wako kwenye jokofu kunahusu kila kitu kwenye jokofu ambacho kinatoa
harufu,” anasema Jack. “Mfuniko wa mvinyo ni kitu cha asili, kwa hivyo
kinapitisha vitu kuingia na kutoka. Maana yake ni kama kuna kipande cha sangara
au kitunguu kwenye jokofu, ni ukweli kuwa mvinyo wako unaenda kuchukua harufu
au ladha za kitunguu au sangara”
Ukifikiria
ni ladha ipi mvinyo wa kitunguu utakuwa nayo, unaweza kuepuka kuweka mvinyo
wako kwenye jokofu. Badala yake amua kuweka kwenye chombo chenye barafu. Au
kuwa na jokofu dogo la kuhifadhi mwinyo pekee, hapo ni kama miaka imeenda na mivinyo
yako imeanza kuwa michungu. Mvinyo ambao haujafunguliwa unaweza kudumu hadi
miaka 100, anasema Jack.
No comments:
Post a Comment