Julius Makongoro mtoto wa kada wa CCM Makongoro
Nyerere, aliyetangaza nia ya kugombea urais ni miongoni mwa watu watano
walionusurika kifo wakiwa kwenye msafara wa mgombea huyo, kufuatia ajali
ya gari iliyotokea mkoani Kigoma.
Makongoro Nyerere hakuwepo
kwenye gari hilo lililopinduka jana saa 4:30
asubuhi eneo la Mwilanvya wilayani Kasulu na kuwajeruhi Julius aliyeumia
kichwani, waandishi Evance Magige (30) wa magazeti ya Habari Corporation,
Cyprian Msiba (35) wa Chanel Ten aliyeumia mabega.Makongoro Nyerere hakuwepo
Wengine ni Fikiri Marumba (35) Katibu Mwenezi wa CCM, aliyejeruhiwa sikio la kushoto, dereva Ally Tesha (37) mkazi wa Arusha. Julius ndiye alikuwa dereva wakati wa ajali.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, hali za majeruhi ni nzuri baada ya kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu na wanatarajiwa kuendelea na safari.
Kamanda Frednand Mtui, alisema gari lililopata ajali ni Toyota Land Cruiser hadtop na kwamba liliacha njia na kupinduka eneo hilo lililoko Mwilanvya barabara ya Kasulu- Kibondo.
Aidha alisema chanzo cha ajali ni vumbi lililomzuia dereva kuona kikamilifu linalosababishwa na magari hayo ya msafara kukaribiana kwenye njia hiyo yenye vumbi jingi. Gari lililopata ajali lina namba T188 BXG.
Mtui alisema msafara huo ulikuwa na magari matatu Alisema majeruhi baada ya kutibiwa na kuruhusiwa waliazimia kuendelea na safari yao ya kwenda Kigoma mjini.
Kamanda Mtui aliwataka madereva wageni wanapoingia mkoani Kigoma kuwa makini kwa sababu barabara zake nyingi ni za vumbi na zenye kona. Aliwashauri kupeana nafasi wasikaribiane ili kila mmoja aweze kuona nyuma na mbele pia.
Alisema hali ya gari hilo ni nzuri na wataendela na safari yao hadi Kigoma mjini kama walivyokusudia.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment