Wanawake katika kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda
wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala
wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka 10.
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa serikali na
watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.
Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba
watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakaazi wakidai kwamba
ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi
,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa
laana kwa mpinzani wake.
No comments:
Post a Comment