Mtu mmoja amekamatwa na polisi akiwa katika harakati za
kutafuta soko la kuuza mtoto mdogo wa dada yake ambaye ana ulemavu wa ngozi
mwenye umri wa miaka sita.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Juma Bwire
alimtaja mtuhumiwa huyo aliyekamatwa juzi kuwa ni Masanja Mwinamila (44), mkazi
wa Ugembe wilayani Nzega.
Kamanda Bwire alisema polisi walipata taarifa za
mtuhumiwa huyo kutafuta wateja ndipo askari walipoweka mtego kwa kujifanya
wanunuzi na kukubaliana naye kufanya biashara kwa kiwango cha fedha
alichohitaji na kudai kwamba mtuhumiwa alitekeleza makubaliano hayo na kwenda
kumchukua mtoto huyo akiwa na mama yake na ndipo askari walipomtia mbaroni.
Kamanda Bwire alieleza kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya
upelelezi kukamilika.
Kamanda Bwire alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni
mkakati maalumu unaoendelea kufanywa na polisi kuwalinda watu wenye ulemavu wa
ngozi.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Joyce Mwandu alieleza kuwa kaka
yake alifika nyumbani kwake na kudai kuwa amekwenda kumtembelea na baada ya
muda alitokomea na mtoto hadi alipopata taarifa za kukamatwa kwake.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment