Najiuliza kama ni sahihi mtoto kuingilia mapenzi ya mzazi..MKAZI wa kitongoji cha Izia, manispaa ya Sumbawanga
mkoani Rukwa, Sylvester Mtoni (32) ameuawa kikatili na baba yake wa kambo
wakishirikiana na bibi yake baada ya kushambulia kwa ngumi, mateke na rungu.
Mtafaruku huo
ulitokea baada ya marehemu kuamua kumfukuza baba yake huyo wa kambo
anayefahamika kwa jina moja la Bea mwenye umri wa miaka 32 akipinga uamuzi wa
mama yake mzazi kuishi nae kinyumba katika nyumba aliyoijenga marehemu baba
yake.
Inaelezwa kuwa
wakati mkasa huo ukitokea mama mzazi wa marehemu alikuwa safarini akielekea
jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa mtoto
huyo alimkatalia mwanamume huyo kumwoa mama yake mzazi kwa kuwa ni kijana
mwenzake umri wao ukilingana ambao ni nusu ya umri wa mama yake mzazi.
Akithibitisha
kutokea kwa mkasa huo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Leonce Rwegasira
alidai kuwa ulitokea juzi usiku katika kitongoji cha Izia Manispaa ya
Sumbawanga.
Alieleza kuwa chanzo
chake ni kuwa marehemu alipinga uamuzi wa mama yake mzazi kuolewa na mwanaume
ambaye ana umri sawa na yeye (Sylivester) na kuishi katika nyumba aliyoijenga
marehemu baba yake.
“Usiku huo wa tukio
mtuhumiwa ambaye anatafutwa na jeshi la polisi alimshambulia mwanawe huyo wa
kambo akisaidiwa na mama mkwe wake wakimpiga kwa ngumi mateke na kipande cha
ubao hadi kijana huyo alipopoteza fahamu,“ alieleza Kaimu Kamanda Rwegasira.
Akifafanua aliongeza
kuwa alikimbizwa Hospitali ya Mkoa ambapo alikufa akiwa anaendelea na matibabu
hospitalini hapo.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment