Mkulima kutoka Kigoma, Elidephonce Bilohe akiondoka baada ya kushindwa kuchukua fomu kutokana na kutokamilisha malipo ya ada ya fomu hizo. Hata hivyo, alikamisha baadaye na atachukua fomu leo Picha na Edwin Mjwahuzi
Makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo wa
darasa la saba, jana walijitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa
na chama hicho wagombee urais.
Waliojitokeza ni Dk Mwele Malecela, Dk Hamis Kigwangalla
na Elidephonce Bilole mwenye elimu ya darasa la saba ambao walifika Makao Makuu
ya CCM kati ya saa nne asubuhi na saa saba kwa staili tofauti kwa ajili ya
kuchukua fomu hizo.
Hata hivyo, Bilole (43) aliyetembea kwa miguu huku akiwa
amebeba chupa mbili za maji, mfuko wa plastiki na begi dogo jeusi, hakuweza
kuchukua fomu kutokana na kufika katika ofisi hizo akiwa hana Sh1 milioni za
malipo.
Baadaye alifanikiwa kulipa ada hiyo na sasa amepangiwa
kuchukua fomu yake leo saa 10.00 jioni.
“Nilikuwa Benki ya CRDB, nikaitwa ofisi za chama nikaona
nije ili nisikilize wito, kabla ya kuchukua fedha kwanza,” alisema Bilole
aliyefika peke yake kwenye ofisi hizo.
Bilole alisema anajua Mungu atamwezesha kukabiliana na
watu wengine walioomba ridhaa ya chama kuwania nafasi hiyo.
Alipoulizwa sababu ya kufika pekee yake katika ofisi
hizo, alisema hajawahi kuwa na makundi ambayo yameonekana kwa makada wengine...
“Nadhani naweza ndiyo maana nimejitokeza kuwania nafasi hii.
Nitawavusha
kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi,” alisema na kuongeza kuwa alijiunga na chama hicho
mwaka 2003 huku akiahidi kuhakikisha anainua uchumi wa nchi kwa kutumia
rasilimali zilizopo.
Bilole ni nani?
Bilole alizaliwa Januari 21, 1971 katika Kijiji cha Mtala
wilayani Kasulu mkoani Kigoma na anajishughulisha na kilimo.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment