Friday, June 5, 2015

Mfahamu Abela Kibira, mwanamuziki Mtanzania Mmarekani anayefanyia kazi zake za muziki Marekani


Mkoa wa Kagera umebarikiwa kuwa na uwakilishi mzuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya nchi, mfano mzuri ni Mwanamuziki wa kike Abela ambaye ni mzaliwa wa Bukoba Mkoani Kagera anayepeperusha vyema bendera ya Tanzania kimziki huko Amerika anakoishi na kufanya kazi zake za muziki.

Abela Kibira alizaliwa Septemba 22 mwaka 1989 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya Mtanzania Josiah Kibira mzaliwa wa Bukoba Kagera, Tanzania na Mmarekani, Mrs Josiah Kibira. 

Mchanganyiko huo wa tamaduni mbili kwa binti huyo ambaye ana kipaji cha utunzi na uimbaji, umemfanya kujimarisha na kujijengea jina katika muziki kutokana na aina ya muziki na manjonjo anayoyafanya katika mzuiki wake kupendwa.

Abela ni mzaliwa wa Bukoba, Tanzania lakini kwa sasa anaishi Minneapolis, Marekani. Binti huyu anasauti nzuri, ya kipekee na ya kuvutia jambo ambalo nyimbo zake nyingi zimekuwa zikipendwa sana
Onyesho lake la kwanza Binti huyu alilifanya kanisani na ndipo kipaji chache kilipojifunua machoni mwa watu wengi na hivyo kuendelea kuimba katika matamasha mbalimbali shuleni na matamasha maalumu.

Abela amekulia katika mji wa Wayzata, Minnesota na alipendwa kutokana na kuwa na uwezo wa ajabu katika kuimba kwaya na matamasha ya pamoja wakati akiwa katika masomo yake ya sekondari na chuo.

Mwaka 2003 baba yake mzazi Mr. Josiah Kibira alimshirikisha katika filamu yake aliyoiita Bongoland, ambapo Abela alitunga wimbo wa kusindikiza filamu hiyo (soundtrack) jambo lililomuongezea uwezo na umaarufu kwa mashabiki Amerika, Afrika na maeneo mengi ulimwenguni.

Abela ambaye bado binti kigoli anayejitambua amekuwa akiimba na kujifua utumiaji wa sauti takriban maisha yake yote lakini kwa sasa amejikita zaidi katika utunzi na utengenezaji wa nyimbo za Hip Hop, Reggae na ni mzuri katika aina tofauti tofauti za muziki.Pia anapendelea zaidi muziki wa bendi hii ina maana kwamba anataka kuonesha kipaji chake.

Abela hana shida juu ya kufanya collabo na wasanii wa Kitanzania na Africa kwa ujumla kwa hiyo kama unapenda kumshirikisha kazi ni kwako! Kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake unaoitwa Ball & Chain.

Kabla ya hapo ametamba na nyimbo nyingi zikiwemo Rolling Stone, Someone like you na Hey Ya.

VIJIMAMBO

No comments:

Post a Comment